Chapter 61 of 150

Zaburi61

Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu.

Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi.

Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui.

Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.

Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi.

Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.

Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.

Zaburi 61 · KJV Audio
0:00
0:00