Chapter 54 of 150

Zaburi54

Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako.

Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.

Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu.

Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.

Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize.

Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema.

Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.

Zaburi 54 · KJV Audio
0:00
0:00