Chapter 131 of 150

Zaburi131

Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.

Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.

Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele.

Zaburi 131 · KJV Audio
0:00
0:00