Chapter 129 of 150
Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:
wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.
Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.
Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.
Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.
Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;
kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.
Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”