Chapter 12 of 24

Yoshua12

Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.

Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi ), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.

Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:

nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

mfalme wa Yerikommojamfalme wa Ai (karibu na Betheli)mmoja

mfalme wa Yerusalemummojamfalme wa Hebronimmoja

mfalme wa Yarmuthimmojamfalme wa Lakishimmoja

mfalme wa Eglonimmojamfalme wa Gezerimmoja

mfalme wa Debirimmojamfalme wa Gederimmoja

mfalme wa Hormammojamfalme wa Aradimmoja

mfalme wa Libnammojamfalme wa Adulamummoja

mfalme wa Makedammojamfalme wa Bethelimmoja

mfalme wa Tapuammojamfalme wa Heferimmoja

mfalme wa Afekimmojamfalme wa Lasharonimmoja

mfalme wa Madonimmojamfalme wa Hazorimmoja

mfalme wa Shimron-Meronimmojamfalme wa Akishafummoja

mfalme wa Taanakimmojamfalme wa Megidommoja

mfalme wa Kedeshimmojamfalme wa Yokneamu katika Karmelimmoja

mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) mmojamfalme wa Goimu katika Gilgalimmoja

mfalme wa Tirsammoja wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

Yoshua 12 · KJV Audio
0:00
0:00