Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.
Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
Eberi alipata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari: Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa: Sheba na Dedani.
Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana.
Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.